Mathayo 28: 18-20
Mshauri ----- Mfariji
Yohana Mtakatifu 14:26
Katika Biblia ya aina ya "New International Version" na ya "Amplified
Version" na zinginezo, neno "Mshauri" limetumika badala
ya "Mfariji".
Inajulikana kwa kila mtu ya kwamba mfariji ni huyo Roho Mtakatifu yaani Roho
wa Kristo aliepaa binguni. Yohana 14:16-18.
Mungu aliye na uwezo
Isaia alimwita kwa jina "Mungu
alie na uwezo".
Ufunuo 1:8
Yesu anajiita mwenyewe "Mungu alie na uwezo wote."
Ufunuo 4:8 na 11:17, walimsujudu yeye na kumwita Baba "Mungu Mweza Yote."
Baba Alie Wamilele
Wakati Yesu alikua duniani alikua
mwenye asili mbili; alikua mwanadamu na pia Mungu; Roho wake ndiye alikua muumba
wa vitu vyote (Yohana 1:3, Wakorosai 1:16,17).
Isaia 44:24 Ya eleza ya kwamba Mungu ndiye aliviumba vitu vyote, yeye mwenyewe
akiwa pekee.
Maandiko haya ya Biblia yadhibitisha ya kwamba Yesu alie Mungu katika agano
jipya ndiye yule aliyekua Mungu katika agano la kale.
Kwa hivyo jina, "Bwana Yesu" ni lazima liwe ndilo jina la Baba, na
la Mwana na tena la Roho Mtakatifu.
Siri ilio kuu
1 Tim. 3:16 Paulo atuzungumizia
juu ya Siri ilio kuu ya Uungu; ya kwamba Mungu alifanyika mtu na akakaa kati
ya wanaadamu.
Soma Yohana 1:14 ni kama fumbo lililo kubwa; Ni lazima tulinganishe vifungu
vyote vya Biblia pamoja ilitupate mfano dhahiri na hasili ya Mungu.
Yohana 14:25,26
Kif. 25 ----"Hiyo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambayo sitasema
nanyi tena kwa mithali; lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba.
Kif. 26 ----" Na siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba
mimi nitawaombea kwa Baba," wakati huu akiwa ametukuzwa na Babake, na hali
yake ya kua "Mungu ndani ya mwili wake" itakua imefika kikomo.
Maandiko yake mariko
Mariko 16:15-17
Yesu aliaamuru mitume wake.
Kif.15 ---Enedeni ulimwengu mwote mkaihubili injili kwa kila kiumbe."
Kif.16 ---"Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiye amini, atahukumiwa."
Kif.17 ---"Kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya,"
Viongozi wengi hodari wakidini hufundisha ya kwamba mtu anaeokolewa kwa kumwamini
Bwana Yesu na kumkubali kama mwokozi; fundisho hili linaweza kuaje haliandamani
na "agizo kuu pamoja na "Amri zake Mungu ---
Kulingana na Maandiko ya Luka
Walimtii Yesu
Yalio Tokea---
Ilio agizo
Matendo 2:14-36----Petro akiwa
ndiye nwenye funguo za ufalme, alihubili ujumbe wa kusandikisha sana kwa ule
umati ulio kusanyika.
Kif.37 ---walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume
wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Kif.38 ---wakati huo "Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa
jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha
Roho Mtakatifu."
Kif.39 ---"A hadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu
wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie."
Rafiki, hata ikiwa ni miaka zaidi ya elfu mbili imepita ujumbe huu una tuhusu.
Kif.41 ---Wale wote walio upokea ujumbe wake Petro walimbatizwa siku hiyo; na
kundi la waaminio likaongezeka na watu elfu tatu.
Mlango Uwazi Kwa Mataifa
Matendo 10:1-48---Kwa maono,
mchaji Mungu aliyeitwa Kornelio alitembelewa na malaika ambaye alimwambia amtume
mtu akamuita Petro. Alimwambia ya kwamba Petro ndiye atakae mueleza yampasayo
kutenda.
Fahamu tafadhali Matendo 11:14
---"atakayekwambia maneno ambayo yatakuokoa wewe na nyumba yako yote."
Kwa wakati ule ule Petro alipata maono kutoka kwa Bwana akionyeshwa ya kwamba
wokovu huu mkuu ulikuwa wa mataifa pia.
Petro alienda nyumbani kwa Kornelio na kumhubiria juu ya Yesu, kifungu cha 44-46
-- "Petro alipokuwa akisema maneno haya Roho Mtakatifu akawashukia wote
waliolisikia lile neno, --- kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha na kumwadhimisha
Mungu."
Ubatizo Ukatika Amri
Vifungu 47-48 ---"Ni nani awezaye kukataza maji, hawa wasibatizwe, watu aliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? Akaamuru wabatizwe, kwa Jina lake Yesu Kristo.
Swali
Je huoni amri hii ina kuelekea
pia, hata ikiwa umepokea Roho Mtakatifu na huja batizwa kwa jina la Yesu?
Kumbuka hakuna jina lingine nduniani limepeanwa liwezalo kutuokoa! (Matendo
4:12).
Kuzaliwa Mara Ya Pili
Yohana 3:3-7 ---Yesu alimwabia Nikodemo yakwamba hangeweza kuona wala kuingia
katika ufalme wa Mungu iwapo haja zaliwa mara ya pili.
Nikodemo akamwuliza Bwana, "Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee?"
Kif.5 ---Yesu akasema, Amini amini nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa
Roho hawezi kwingia ufalme wa Mungu.
Kif.7 ---Yesu mwenyewe aliitamka amri, "Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
Rafiki ukweli wa neno la Mungu umekwishawekwa mbele yako; sasa ukweli u mikononi
mwako; usiupinge.
Apostolische
Pfingstgemeinde (UPC) Friedelsheimer Str. 14-20 68199 Mannheim Germany http://www.v-p-m.de |
Worship
Service: Sunday 2.30 pm Biblestudy: Tuesday 7.00 pm |