Neno La Mungu
Limewekwa Wazi
NENO LAKO NDIYO
UKWELI. . . . " Yohana 17:17
"TENA MTAIFAHAMU KWELI, NAYO HIYO KWELI ITAWAWEKA HURU." Yohana
8:32
HITAJI LA WANADAMU LA WOKOVU
"Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu."
Warumi 3:23
Kutoka
Mwanzo:
Adamu Na Hawa
* BUSTANI YA EDENI
* DHAMBI YA KUTOTII
HUKUMU: Kufukuzwa . . . Kazi . . . Maumivu. . . . Hatia
Dhambi ni URITHI
"Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba
hatiani." Zaburi 51:5
"Hakuna mwenye haki hata mmoja." Warumi 3:10
"Basi mwanadamu wa tabia ya asili” (ambaye hajaokoka) ”hayapokei
mambo ya Roho wa Mungu. . . ." 1 Wakorintho 2:14
MWANADAMU
HAWEZI KUJIOKOA MWENYEWE!
KAZI ZETU
"Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa
rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.”
Tito 3:5
HAKI
YETU
"Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu na
matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi. . . .”
WEMA WETU:
". . . Hakuna aliye mwema ni mmoja. . . .” Naye ni Mungu.
Mathayo 19:17
DINI YETU:
"Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele
zake kwa matendo ya sheria. . . ." Warumi 3:20
"Hali tukijua ya kuwa mwanadamu, hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria,
bali kwa imani ya Kristo Yesu. . . ." Wagalatia 2:16
HAYAWEZI KUTUOKOA |
MUNGU
PEKEE NDIYE NAYEOKOA |
KIPAWA
CHA MUNGU CHA WOKOVU
KWA NJIA YA KRISTO:
"Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote...."
Matendo 4:12
". . .Na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo." Waebrania 9:22
MTIRIRIKO
WA DAMU
"Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu....” Isaya 53:5
SHERIA:
Mungu
aliyompa Musa Mlima Sinai.
SHERIA ZA SHEREHE :
* MAKUHANI
* DHABIHU
* DAMU
KUELEKEZA
KALVARI:
"Mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo. . . ." Wakolosai
2:17
"Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo. . . ." Wagalatia
3:24
SHERIA HAIKUWA YA KUDUMU
"Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria.
. . ." Wagalatia 3:11
"Kristo alitukomboa katika laana ya torati,. . . ." Wagalatia 3:13
"Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana. . .tangu wakati huo habari njema
ya ufalme wa Mungu hutangazwa. . . ." Luka 16:16
MWANA KONDOO :
YOHANA ALIMTAMBULISHA: “. . . Tazama Mwana-kondoo
wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" Yohana 1:29
ALIKUWA: ". . . Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu
kuwekwa misingi ya dunia." Ufunuo 13:8
". . . Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima
na nguvu na heshima na utukufu na baraka." Ufunuo 5:12
KUZALIWA
KWAKE: KULITANGAZWA NA MALAIKA: "Maana leo katika mji
wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi ndiye Kristo Bwana." Luka
2:11
MAISHA YAKE: ". . . Naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema
na kuponya wote walioonewa na Ibilisi. . . ." Matendo 10:38
ALISEMA:
"Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima. . . ." Yohana 14:6
"Mimi ndimi mlango, mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka,
naye atapata malisho." Yohana 10:9
"Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake."
1 Petro 2:22
KIFO
CHAKE: "Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka
mahali paitwapo . . . Golgotha wakamsulubisha huko. . . ."
Yohana 19:17-18
". . . Kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye
dhambi." Warumi 5:8
"YAMEKWISHA."
Yohana 19:30
Kilio Kutoka Msalabani
Mpango wa Mungu Kuokoa
MAZIKO:
“Naye . . . akamfungia ile sanda, . . . lililochongwa mwambani. . . ."
Marko 15:46
UFUFUKO: “. . .Mnamtafuta Yesu . . aliyesulubiwa;
amefufuka." Marko 16:6
KUPAA: ". . . Wingu likampokea kutoka machoni pao."
Matendo 1:9
KANISA:
* KANISA NI USHIRIKA WA WAAMINI WALIOBAPTIZWA NA
AMBAO WAMETII MPANGO WA WOKOVU WA MUNGU.
* KUNA KANISA MOJA TU: "MWILI MMOJA" Waefeso 4:4
"IMANI MOJA" Waefeso 4:5
LILIAHADIWA:
“... Na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya
kuzimu haitalishinda." Mathayo 16:18
SIKU CHACHE KABLA
YA PENTEKOSTE ALIAHIDI: “. . . Bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu
baada ya siku hizi chache." Matendo 1:5
LILIANZISHWA: "Hata ilipotimia siku ya Pentekoste
walikuwako . . . . Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha
nyingine, kama Roho alivyowajaliakutamka." Matendo 2:1-4
LILIFUNGULIWA:
". . .Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo
la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Matendo 2:38
"Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote
walio mbali. . . ." Matendo 2:39
KANISA LIKO WAZI: ". . . na yeye atakaye. . . ."
Ufunuo 22:17
TUKIO:
Yesu alisema: ". . . Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia
ufalme wa Mungu." Yohana 3:5
HAYA YALITAFSIRIWA NA KUELEZEWA KATIKA UJUMBE WA PETRO KATIKA MATENDO YA MITUME.
"Mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu." Matendo 2:38
WAYAHUDI:
Matendo 2:4
"Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine,
kama Roho alivyowajalia kutamka."
WASAMARIA:
Matendo 8:15-17
". . . Wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia
hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu . . nao wakampokea
Roho Mtakatifu."
MATAIFA:
Matendo 10: 44-48
". . . Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno."
(aya 44) Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja
pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha. . . . Ni nani awezaye kukataza
maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?
Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. . . ."
WATU
WA DINI: Matendo 19:2-6
". . . Je! mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La. . . .
" (aya 2) "Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
. . . Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri."
WOTE WALITUBU NA KUAMINI | WOTE WAKABATIZWA KWA JINA LA YESU | WAKAJAZWA NA ROHO MTAKATIFU NA KUNENA KWA LUGHA MPYA |
". . . NITAMIMINA ROHO
YANGU JUU YA WOTE WENYE MWILI... ." Yoeli 2:28
YESU:
“YHVH . . . AMEKUWA WOKOVU WANGU.” Isaya 12:2
(Marejeo ya Maandiko Luka 1:77; 2:30; 3:6)
MUNGU ALIKUWA NA VYEO VINGI LAKINI KWENYE UKOMBOZI NI JINA MOJA
TU.
"Naye
BWANA atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja
na jina lake moja." Zekaria 14:9 ". . . Naye akasema, Mimi ndimi Yesu. . . ." Matendo 9:5 ". . . Naye ataitwa jina lake, Mashauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani." Isaya 9:5 |
“. . . Jina lile lipitalo kila jina . . . Wafilipi 2:9 |
JE! BIBLIA
INASEMA NINI KUHUSU ONDOLEO LA DHAMBI?
". . . Mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la
dhambi. . . .” Matendo 2:38
". . . Ya kwamba kwa jina lake . . . atapata ondoleo la dhambi." Matendo
10:43
". . . Watahubiriwa kwa jina lake . . . ondoleo la dhambi. . . ."
Luka 24:47
JE! YESU ALIAMURU UTUMIAJI WA JINA LAKE KATIKA MPANGO WA INJILI?
". . . Na
kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo
la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu." Luka 24:47
". . . Mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina.
. . . “ Mathayo 28:19
JE! MITUME WALIMTII?
"Petro akamwambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina
lake Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi. . . . " Matendo 2:38
"Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. . . ." Matendo
10:48
". . . Wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu." Matendo 8:16
TUNAJIHUSISHA SISI WENYEWE NA JINA LA YESU NA KULICHUKUA JINA LAKE KWA KUTII TUNAPOBATIZWA KWA KULINGANA NA MAANDIKO.
UKWELI
WA MAANDIKO:
"Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana
hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi
kuokolewa kwalo." Matendo 4:12
"Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina
la Bwana Yesu...“ Wakolosai 3:17
UKWELI WA HISTORIA:
"Kanisa la mwanzo kila mara lilibatiza katika Jina la Bwana
Yesu . . . ." Canney Encyclopedia. Uk. 53
"Mpangilio wa kwanza wa maneno ulikuwa ‘Katika jina la Yesu Kristo
au Bwana Yesu.’" Kubatizwa katika Utatu ilikuwa tukio lililo
kuja baadaye. Kamusi ya Biblia na Scribners, Uk. 241.
BASI
SASA, UNAKAWILIA NINI? SIMAMA, UBATIZWE, UKAOSHE DHAMBI ZAKO, UKILIITIA
JINA LAKE." Matendo 22:16 |
·
MUNGU NI WA HALI YA AINA GANI? · YESU KRISTO ALIKUWA NANI? · ROHO MTAKATIFU NI NANI? · KANA UTATU (TRINITY) |
HAYA NI MASWALI AMBAYO KILA MTU ANATAKIWA AYAJUE MAJIBU YAKE. |
ONA
UTHABITI WA MUNGU: “Ni Roho”
NENO “ROHO” LIKO KWENYE UMOJA, KUSISITIZA UKWELI KWAMBA MUNGU
SI WINGI WA NAFASI.
"KUNA
ROHO MMOJA!" Waefeso 4:4 MUNGU!
Kuthibitisha Marko 12:29: ". . . SIKIA, ISRAELI, BWANA MUNGU WETU NI
BWANA MMOJA!"
". . . Mimi ni BWANA, Mtakatifu wenu!" Isaya 43:15
"Je! yuko Mungu zaidi yangu mimi? . . . MIMI SIJUI MWINGINE." Isaya 44:8
“MUNGU
(ROHO) ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI . . . ."
LINI?
* Mathayo 1:23: ". . . Imanueli;
. . . Yaani, Mungu pamoja nasi."
* Waebrania 10:5: ". . . Lakini
mwili uliniwekea tayari. . . ."
* Waebrania 1:3: "Yeye . . . ni
. . . chapa ya nafsi yake."
* Luka 1:35: “. . . Hicho kitakachozaliwa
kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu."
* Isaya 9:6: "Naye ataitwa jina
lake . . . Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfame wa amani."
* Waebrania 2:16: "Maana ni hakika,
hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu."
* Wakolosai 2:9: "Maana katika yeye
unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili."
YESU KRISTO ALIKUWA MUNGU NA PIA MWANADAMU:
KAMA MWANADAMU: ALISIKIA NJAA, KUCHOKA, AKATOA MACHOZI.
KAMA MUNGU: ALIFUFUA WAFU, AKATULIZA MAWIMBI YA BAHARI, ALISAMEHE DHAMBI.
". . . YESU HUYO . . . KUWA BWANA NA KRISTO." Matendo 2:36
BABA KATIKA UUMBAJI MWANA KATIKA UKOMBOZI ROHO MTAKATIFU KATIKA KUZALIWA UPYA |
“Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka." Yakobo 2:19
(Marejeo ya Maandiko: Kutoka 2:14-16; Kumbukumbu la Torati 6:4-6; Isaya 44:6; Isaya 45:5-6, 21-22; Isaya 48:11; Yohana 1:1-3,14; Warumi 3:30; 1 Wakorintho 1:8)
HEBU
TUANGALIE KATIKA USHUHUDA WA:
MANABII:
". . . Naye ataitwa jina lake . . . Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele,
Mfalme wa amani." Isaya 9:6
". . . Bali Bwana ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme
wa milele. . . ." Yeremia 10:10
". . . BWANA atakuwa mmoja . . . na jina lake moja." Zekaria 14:9
MALAIKA:
"Maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi,
ndiye Kristo Bwana." Luka 2:11
MITUME:
"Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja." Waefeso 4:5
". . . Mungu alidhihirishwa katika mwili. . . ." 1 Timotheo 3:16
"Maana katika yeye” (Yesu) “unakaa utimilifu wote wa Mungu,
kwa jinsi ya kimwili." Wakolosai 2:9
"Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!" Yohana
20:28
YESU MWENYEWE:
“Mimi na Baba tu umoja.” Yohana 10:30
“Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia,
Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona
mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?” Yohana 14:8-9
“Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. . . .” Ufunuo 1:11
MAISHA YA KIKRISTO
KUISHI KWA KITAUWA NA UTAKATIFU SHARTI UFAFANISHE MAISHA YA KILA MWAMINI
"Maana neema ya Mungu iwaokoayo … nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa." Tito 2:11-12 |
“Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu" 1 Petro 1:16
DHAMBI
". . . Dhambi ni uasi." 1 Yohana 3:4
"Kila lisilo la haki ni dhambi. . . ." 1 Yohana 5:17
"Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa
milele . . . .” Warumi 6:23
"Atendaye dhambi ni wa Ibilisi. . . " 1 Yohana 3:8
KAMA MTU ATATENDA DHAMBI MARA MOJA TU KILA SIKU NA UMRI WAKE NI:
MIAKA 20 atakuwa na dhambi 7,300 MIAKA 30 atakuwa na dhambi 10,950 MIAKA 40 atakuwa na dhambi 14,600 MIAKA 50 atakuwa na dhambi 18,250 MIAKA 70 atakuwa na dhambi 25,550 |
SIKU YA HUKUMU |
"Msipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele." 1 Yohana 2:15-17
UTAKATIFU
NI NJIA YA MUNGU
"Tafuteni . . . utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana
asipokuwa nao." Waebrania 12:14
"Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa
watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima
wa milele." Warumi 6:22
FURAHA
"Lakini tunda la Roho ni . . . furaha . . . ." Wagalatia 5:22
". . . Na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu."
1 Petro 1:8
"MAANA UFALME WA MUNGU
SI KULA WALA KUNYWA, BALI NI HAKI NA AMANI NA FURAHA KATIKA ROHO MTAKATIFU."
WARUMI 14:17
Kuja Kwa Kristo Mara
Ya Pili
"Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena.
. . ." Yohana 14:3
"…Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja
jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni." Matendo 1:11
TUMAINI LILILO BARIKIWA LA MKRISTO
"Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu,
Mungu mkuu na Mwokozi wetu." Tito 2:13
WAKATI WA
KUJA KWAKE:
"Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye. . . ." Mathayo
24:36
"...Kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja."Mathayo 24:44
KITU MUHIMU: KUJITAYARISHA KWETU
"Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari. . . ." Mathayo 24:44
HAKUTAKUWA NA WAKATI TENA |
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; . . . kwa kuwa mambo ya kwanzo yamekwisha kupita.” Ufunuo 21:4 |
WASIOAMINI NA WASIOTII: MUNGU HAFANYI MCHEZO NA DHAMBI!
“Bali waoga,
na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo
sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti.
Hii ndiyo mauti ya pili." Ufunuo 21:8
"Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye
afanyaye machukizo na uongo. . . ." Ufunuo 21:27
"Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi
ataonekana wapi? 1 Petero 4:18
JE! MWENYE DHAMBI NI NANI?: MTU ANAYEPAKA RANGI NI MPAKA-RANGI; NA MTU ANAYECHOMEA NI MCHOMEAJI; MTU ANAYETENDA DHAMBI NI MMENYE DHAMBI! |
"Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo."
Luka 13:3
". . . Wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na
malaika wa uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua
Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu." 2 Wathesalonike 1:7-8
"KWA
MAANA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI.” Warumi 6:23
...Ziwa la moto... Ufunuo 19:20
KWA HIVYO UNAONA SHARTI TUFANYE UAMUZI WETU LEO!
"Tazama, wakati uliokubalika ndio
sasa . . . siku ya wokovu ndiyo sasa." 2 Wakorintho 6:2
UKARIBU WA MTU KWA WOKOVU HUTEGEMEA KUWA KWAKE RADHI KUKUBALI NA KUTII NENO LA MUNGU!
* UNAJALI NA NAFSI YAKO?TOBA |
Sodoma na Gomora Yona Yohana Mabtizaji Yesu Kristo Agizo Kuu Siku ya Pentekoste |
Mwanzo 19; 2 Petro 2:6; Yuda 7 Mathayo 12:41 Mathayo 3:2 Luka 13:3 Luka 24:47 Matendo 2:38 |
UBATIZO WA MAJI MENGI – KATIKA JINA LA
YESU |
Yerusalemu Samaria Kaisaria Efeso |
Matendo 2:38 Matendo 8:16 Matendo 10:48 Matendo 19:1,5,6 |
UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU – ISHARA: WALINENA
KWA LUGHA NYINGINE |
Yerusalemu Kaisaria Ushuhuda wa Petro Efeso |
Matendo 2:4 Matendo 10:44-48 Matendo 11:15-18 Matendo 19:1, 5, 6 |
Apostolische
Pfingstgemeinde (UPC) Friedelsheimer Str. 14-20 68199 Mannheim Germany http://www.v-p-m.de |
Worship
Service: Sunday 2.30 pm Biblestudy: Tuesday 7.00 pm |